SHARE

Panya, mende, wadudu na vyoo vilivyovunjika ni miongoni mwa vitu vingi vilivyoripotiwa kwa wafanyakazi wa kufanya marekebisho katika Ikulu ya Whitehouse nchini Marekani.

Ripoti ya vitu vinavyofaa kurekebishwa katika Ikulu ya White house iliyopatikana na chombo cha habari cha NBC Washington ilishirikisha ripoti nyengine ya mwaka uliopita kutoka kwa utawala wa rais Obama ilibainisha kuwa panya na wadudu hao huonekana katika idara mbalimbali zilizomo Ikulu

Panya wanadaiwa kuonekana katika chumba cha kulia chakula cha maafisa wa jeshi la wanamaji.

Walionekana katika majengo, kulingana na taaria iliyotolewa na Brian Miller, aliyekuwa inspekta jenerali wa kikosi cha huduma za jumla ambacho husimamia marekebisho katika jumba hilo la rais.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here