SHARE

Tasnia ya michezo na siasa nchini imepata pigo baada ya hii leo aliyekuwa ,Kocha,Mbunge,Waziri wa Michezo na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera kufariki dunia.

Bendera ambaye atakumbukwa kwa wengi hasa wadau wa michezo nchini kwa kuiwezesha timu ya taifa Taifa Stars kufuzu kwa mara ya kwanza na mwisho michuano ya kombe la Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria,amefikwa na mauti hii leo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Aidha katika medani za siasa nchini,Mzee Bendera atakumbukwa na wengi kwa kuwa miongoni mwa waliounda maraza la mawizi katika serikali ya awamu ya nne,akiwa kama waziri a habari na michezo.

Pia ,Bendera alipata bahati ya kulitumikia taifa katika nafasi ya Ukuu wa mkoa,ambapo mara ya mwisho alikuwa mkuu wa mkoa wa Manyara,kabla ya hivi karibuni kuwekwa kando na Rais Magufuli katika teuzi alizozifanya .

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here