SHARE

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe  amekutana na wasanii wa tasnia mbalimbali hapa nchini na kumzungumza nao juu ya ujio wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ inayotarajiwa kuzinduliwa Disemba 8 mwaka huu huko mkoani Dodoma.

Waziri huyo aliwataka wasanii kuendeleza  na kuutangaza uzalendo wetu unaoendana na maadili yetu, ikiwa kauli mbiu ni ‘Nchi Yangu Kwanza’.

Amesema hayo  jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa uwanja wa Taifa akiwahimiza Wasanii hao ambao ni kioo cha jamii kuwa na  mchango mkubwa  katika kuijenga nchi yetu.

‘Mrisho ndiye aliyesababisha sisi kuwa hapa, alileta wazo na sisi tumelishughulikia na sasa hivi limekuwa wazo kubwa hata mwenyewe haamini. Kwahiyo sisi tumewaita hapa kwaajili ya kampeni hii ambayo inakwenda kulikomboa Taifa letu. Waandishi wa habari pia ni miongoni mwa mashujaa wetu waliotufikisha hapa tulipo” amesema waziri Mwakyembe.

Waziri  Mwakyembe  amesema kuwa siku ya Ijumaa 8, Desemba mwaka huu  Dodoma kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kampeni ya uzalendo kwanza kwa nchi yangu ambapo uzinduzi huo  utahudhuruwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa ni mzalendo wa kwanza katika ujenzi wa taifa letu.

Aidha Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na michezo Juliana Shonza  amesikitishwa na baadhi ya wasanii ambao ni vioo vya jamii hapa nchini kutokuwa na maadili ya kizalendo kwa kutumia vibaya vyombo vya mawasiliano  kwa kupiga picha zisizofaa na kutuma kwenye mitandao ya kijamii,Na amewataka kuwa  mabalozi wazuri katika  kutangaza uzalendo kwanza Hapa nchini

Hata hivyo naibu  huyo  ametoa pongezi za dhati kwa  Mrisho mpoto akiwa mzalendo alietoa wazo hilo na wasanii wenzake, Na amesema kuwa  wizara imeipa uzito kampeni hii na kuamua kuwa inde mkoani kwaajili ya uzinduzi huo.

Vile vile pia naibu Shoza  amempongeza mwanamashumbwi Ibrahim class kwa kuwa mzalendo kwa kuwa bingwa wa 3 barani Afrika na   asie na mpinzani  nchini Tanzania na kumkabidhi hundi ya shilingi milioni 18 laki 2 na 40 elfu.

Nae bondia Ibrahimu class  amemalizia kwa kusema kuwa mazoezi na kujiamini ndio kinachomfanya afanye vizuri katika mashindano yake ya ndani na  nnje ya nchi na ametoa shukrani zake za dhati kwa watanzaia kwa kumuunga mkono katika mapambano yake.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here