SHARE

MWANZONI ishu yake ya kutakiwa na Yanga ilichukuliwa poa na watu wakadhani ni zile stori za kipindi cha usajili tu, lakini kumbe mabosi wa Jangwani wamepania kweli kumbeba kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin.

Yanga sasa imeonekana haina mzaha katika ishu ya kumsajili kiungo huyo aliyepo Kenya na kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya Kombe la Cha-lenji.

Yanga wamemzukia huko huko kumalizana naye.Taarifa za kunyapia ambazo zimepatikana ni kwamba Yanga imetuma vigogo wake Kenya ili kuzungumza na Mzamiru huku mkononi wakiwa na mkataba wa awali waliomwandalia.

Mzamiru aliyesajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar, mkataba wake umebakiza miezi sita, hivyo kikanuni anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine yoyote na kuingia nayo maku-baliano ya awali.

Yanga na Azam ndizo zilizoonyesha nia ya kumnasa mapema.Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jangwani, ni kwamba Yanga im-emtengea dau la Sh65 milioni ili kumshawishi kiungo huyo mkali wa mabao.

Pia katika kumweka sawa zaidi, wamekubali kumlipa mshahara wa Sh4.5 milioni kwa mwezi, kumpatia nyumba ya kuishi na gari alilohitaji.Chanzo hicho kinasema, Mzamiru aliyeifungia Simba mabao 12 katika mashindano yote tangu ajiunge nayo, anaonekana kuwa na woga kutokana na simu anazopigiwa na vigogo wa Simba wanaohoji juu ya harakati zake hizi za kutua Jangwani.

“Kuna kigogo wa Yanga alimpigia simu Mzamiru na kumwambia kuna mtu wanamtuma Kenya, wangeon-gea naye baada ya mechi yao na Lib-ya na kweli baada ya hapo, akafuatwa na kupewa huo mkataba na pesa, lakini mpaka sasa bado hajafanya maamuzi yoyote,” alisema mmoja wa watu wa karibu wa Mzamiru na kuomba hifadhiwa jina lake.

Hata hivyo, Yanga inataka kwanza kuona nakala ya mkataba wa Mzamiru na Simba ili kujiridhisha kama ni kweli unamalizika Mei mwakani.

Yanga wakiwa wana-pambana ili kumalizana na kiungo huyo huko Kenya, kuna habari kwamba Kocha Msaidizi wa Bidvest Wits ya Afrika Kusini, Paul Johnstone, naye yupo katika michuano hiyo kwa ajili ya kumfuatilia pia kiungo huyo wali-yevutiwa naye kupitia michuano ya COSAFA iliyofanyika mapema mwaka huu.

Wiki iliyopita, Mzamiru alisema kuwa anahitaji Sh70 milioni, gari na nyumba ya kuishi ili kusaini katika timu yoyote mpya inayohitaji huduma yake, hasa baada ya Yanga na Azam kumfuata.Kiungo huyo alisisitiza kuwa nia yake ni kusonga mbele kisoka, hivyo atajiunga na timu itakayompa nafasi kubwa.

Alikiri pia kuzisikilizia timu kad-haa za nje, hasa kutoka Afrika Kusini.Yanga inamtaka Mzamiru ili akapewe mikoba ya Thabani Kamu-soko ambaye kwa sasa amekuwa na majeraha ya mara kwa mara.

Kwa upande mwingine, Azam inamtaka akazibe nafasi ya Salum Aboubakar ‘Sureboy’ ambaye sasa umri umeanza kumtupa mkono na kasi yake uwanjani imeshuka, hivyo wameona wanahitaji damu mpya inayochemka.

Credit – Mwanaspoti


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here