SHARE

BAADA ya mwanadada ‘lejendari’ kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ kufanya vyema na Ngoma ya Together Remix akiwa na mpenzi wake, Spicy, staa huyo amejipanga kutengeneza naye ngoma tena.

Akichonga na Showbiz ya GP, Jay Dee alisema kwamba ameamua kurudi tena na Spicy na ngoma mpya ya Baby baada ya kolabo ya Together Remix kufanya vizuri ambapo anaamini itampeleka mbali zaidi kimuziki kuliko alipo kwa sasa.

“Nimeamua kumganda Spicy kwa sababu ninaamini ni mwanamuziki mzuri na muungano wetu huwa unafanya vizuri, angalia ngoma iliyopita na hii utagundua kwamba tunapokuwa pamoja tunatengeneza kitu kizuri sana,”alisema Jay Dee.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here