SHARE

Mbunge wa zamani wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM.

Mkosamali amesema ana imani na upinzani imara. Ametaka kupuuzwa kwa taarifa kuwa anakwenda CCM kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli.

“Msimamo wangu upo palepale na kama wamezusha ni wao na sababu zao. Watu wamenipigia simu kuniuliza kuhusu jambo hili. Sijaeleza lolote kuhusu kuhama NCCR. Watanzania tunahitaji upinzani imara, kuhama hatumsaidii Rais unaweza kumsaidia ukiwa hukuhuku upinzani,” amesema.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here