SHARE

Nikamuacha mzee Mikausho akienda kuongea na Sauda huku mimi nikiendelea na kazi zangu huku nikingojea usiku ufike nifanye mambo yangu.

Hatimaye usiku ukafika, na muda wa Magugi kupata chakula ukawa umekaribia, lakini sikuwa nimeonana na mzee Mikausho hivyo sikuwa nikijua kama safari imeandaliwa au laa, nikabaki njia panda nisijue cha kufanya, ingawa mkate wangu nilikuwa nimeusaga tayari, niikuwa nangojea chakula kiwe tayari tu ili niweze kukichanganya na unga wa mkate ule na kumpelekea Magugi.

Kutokuonekana kwa mzee Mikausho kukaninyima uhuru wa kuendelea na kilichopangwa, nikaamua kuahirisha zoezi. Chakula kikawa tayari nami nikawa najiandaa kwenda kukichukua kwaajili ya kumpelekea Magugi bila kuweka ile dawa yangu, lakini wakati nikielekea kuchukua chakula nikakutana na mzee Mikausho ambaye alinipa ishara nimfuate, nami nikamfuata mpaka eneo la mafichoni kidogo ambapo tulisimama. “mkeo anaumwa aisee, tumbo linamsumbua toka jana” alieleza mzee Mikausho, habari ambazo zilinishtua na kunifanya nitamani kumuona mke wangu, “vipi kuhusu kumbukumbu zake? Zimerejea?” niliuliza. “kumbukumbu zake ziko sawa, na anatamani sana kuonana na wewe, ila tunajiuliza ataiweza mikikimikiki ya safari na hali yake ya ujauzito na kuumwa?” alihoji mzee Mikausho. “leo tunaondoka kwa hali yoyote” nilitoa jibu fupi na mzee Mikausho akakubaliana na mimi, ikanibidi kurudi chumbani ambapo nilichukua kale kafimbo na ule unga wangu nikaja kuchanganya kwenye kile chakula huku nikisaidiana na mzee Mikausho. Kila kitu kikawa sawa, nikaenda mpaka kwa Magigi ambaye alikuwa tayari akisubiri chakula “leo chakula kimechelewa kwa dakika 20” alisema Magugi huku akinitizama machoni wakati nikimnawisha, mara zote hupenda kumtizama mtu kwa makini machoni kujribu kuona kama ana dhamira mbaya juu yake, na kama mtu anakuwa na dhamira mbaya lazima ataaingiwa na uoga na pumzi yake kubadilika na Magugi hugundua haraka, lakini kwangu hakuwa akifanikiwa kwamaana mara zote huenda mbele yake mara baada ya kumeza ile dawa yangu na kuzuia kupumua.

Magugi akala chakula kile bila kushtukia chochote, alipomaliza akaonekana kunitizama sana, mpaka nikaanza kuingiwa na wasiwasi “chakula cha leo kilikuwa kitamu sana, kweli mambo mazuri hatayaki haraka” alisema Magugi wakati namnawisha. “umekuwa ukifanya kazi yako vizuri sana mpaka natamani kukuzawaidia, ungependa nikupe zawadi gani?” aliuliza Magugi, nikajiuliza ni akili yake au dawa inafanya kazi, kwa maana hakuoneekana kama mtu ambaye anaweza kufikiri chochote juu ya mtu mwingine. “ningeshukuru kama ungeniambia mlango wa kutokea Muifufu unafuguliwaje” nilijibu nikiwa na wasiwasi maana nilijua kama dawa ile haikuwa imefanya kazi swali lile lingeniweka pabaya. Kabla haasema chochote Magugi akamtizama jini yule ambaye mara zote husimama kando yake, kisha akasema “ni mimi na huyu mlinzi wangu pekee ndio tunajua siri ya kufungua Mlango wa Muifufu, ila kwakuwa ndio zawadi pekee uliyoiona na wewe nitakujuza” aliweka kituo kidogo kisha akaendelea “watu wengi wanatamani kuujua ufunguo wa Muifufu, hawajui kama ufunguo wa Muifufu ni mimi mwenyewe na siku nikifa mlango wa Muifufu utakuwa umefungwa milele” alisema Magugi maneno ambayo yalinishtua. “unamaanisha nini?” niliuliza kutaka ufafanuzi zaidi “mimi ndiye ninayajua maneno ambayo nikiyasema mlango unafunguka, na hata kama mtu mwingine kiyajua maneno hayo hayawezi kumfaa chochote kwani hayatendi mpaka niyatamke mimi, uhai wa mlango wa Muifufu pia umeungana na uhai wangu, siku nikifa basi mlango ule utajifunga na hautofunguka tena” alielezea vizuri Magugi.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here