SHARE

Rais wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori ameachiwa huru kwa msamaha wa Rais wa sasa wa nchi hiyo, Pedro Pablo Kuczynski baada ya kutumikia kifungo chake kwa miaka takribani 12 (tangu 2005).

Fujimori alifungwa kwa kukutwa na hatia ya kupokea Rushwa na kukiuka haki za binadamu. Akiwa hoi kutokana na presha, Fujimori mwenye umri wa miaka 79 amewahishwa hospitali kwa matibabu ya kina.

Duru za siasa nchini humo zinadai kuwa msamaha huo umechochewa na vuguvugu la kisiasa kutoka kwa wapinzani wa Rais aliye madarakani ambao walidhamiria kuwasilisha hoja ya kumng’oa madarakani kwa tuhuma kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya ujenzi ambapo amejitetea kuwa fedha hizo ni malipo ya ada ya ushauri wa kitaalamu.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here