SHARE

MKALI wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka sababu iliyompelekea kushindwa kupiga show katika mji ambao anatokea Rais John Pombe Magufuli, Chato Mkoani Geita na kudai kuwa alishikwa na homa kali na kushindwa kuhudhuria katika show hiyo.

Licha ya Alikiba kushindwa kutokea kama ‘Special Appearance’ katika show ya ufunguzi wa JS Hotel mjini hapo lakini mdogo wake ambaye ndiye alikuwa na show Abdukiba alikinukisha na kuwakosha mashabiki waliotokeza kwenye ‘party’ hiyo.

“Juzi nilitakiwa kujiunga na mashabiki wangu wa chato Geita, nyumbani kwa Baba yetu Muheshimiwa Rais lakini nilishikwa na homa kali ila leo naendelea Vizuri samahani kwa kutokuwepo lakini nawaahidi nitarudi tena kwa nguvu zote Mungu akipenda hivi karibuni tutawaandalia show ya kipekee lakini vilevile Abdukibaa mdogo Wangu aliniwakilisha vema namshukuru sana ” aliandika Alikiba.

Mbali na hilo Alikiba amedai hali yake kiafya sasa iko poa kwani anaendelea vyema na kudai wanajipanga kuona jinsi gani wanaweza kufungua mwaka vizuri 2018 kutokana na kuugua kwake kuharibu mipango yake ikiwa pamoja na kushindwa kufanyika kwa funga mwaka na Alikiba.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here