SHARE

Sasa tutawezaje kuondoka kama baada ya kumuua Magugi mlango utajifunga?? nilijuiliza, lakini sikupata jibu, mwisho nikaamua kubadili mpango. Mpango mpya ukawa kumwambia Magugi aufungue mlango ubaki wazi ili tutumie muda ule usiozidi saa moja kutoroka kabla dawa ile haijamuisha akilini. Jambo pekee ambalo lilibaki kuwa tatizo ni ahadi niliyowekeana na watu wa mlima Kalingisi, watu wale walivunja mwiko wao ili kunisaidia mimi, kuvunjika kwa mwiko huo kunawasababishi wao laana, pengine wamekwishageuka Masokwe kama wale wenzao na wananitegemea mimi kumuua Magugi ili laana hiyo ifutike, lakini sasa sikuwa na nafasi ya kumuua Magugi, potelea mbali natatua kwanza tatizo lililopo mbele yangu, hayo mengine tutajua baadae. “sasa leo ungeuacha mlango wazi angalau hewa iingie kidogo maana mlango ule umekuwa ukifungwa tu siku zote” nilimwambia Magugi naye hakubisha, akayaona maeneno yangu yalikuwa ya busara kweli, akasimama na kunyoosha mikono yake juu huku akisema maneno ambayo sikuyajua maana yake na wala siyakumbuki tena, ndani ya sekunde chache akawa amemaliza na kusema tayari mlango uko wazi, wacha hewa iingie leo.

Hapo nikona tayari nilikuwa nimemuweza, nikaaga kuwa nilikuwa nakwenda kulala lakini nikaenda kwa mzee Mikausho nikamueleza kilichotokea, akafurahi sana na kunitaka tuharakishe mpaka eneo ambalo walikubaliana na Sauda kuwa tutawakuta hapo, kweli tuliwakuta wakiwa wamejificha wakitungojea sisi, mke wangu alifurahi kuniona akajitahidi kusimama na kunikumbatia kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nami nalifurahi sana kumuona akiwa katika akili yake timamu. Kila mtu alikuwa na hamu ya kujua nini kiitokea lakini tukawataka kuondoka kwanza kwani tulikuwa nje ya muda, mengine wangeyajulia huko mbele ya safari. Tulikuwa jumla ya watu tisa ambao ni mimi, mke wangu, Sauda, mzee Mikausho, yule binti wa hakimu ambaye liifunika kesi yangu na kunitaka nimrejeshee binti yake, Hisham na vijana wengine watatu ambao sikuwa nimeyajua majina yao. Yule mzee ambaye alituelekeza kwenda kupata msaada kwa mzee Mikausho yeye niliambiwa aliikataa safari ile akidai anauona mwshilio mbaya mbele ya safari, hivyo wakampuuza na kumuacha na maisha yake ya Muifufu.

Mwendo wetu haukuwa wa kasi sana kutokana na kuwa na mke wangu ambaye alikuwa na mgonjwa pia binti yule wa hakimu ambaye mimba yake ilionekana kufikia mwishoni, hivyo walikuwa na mwendo wa kujivuta huku mimi nikimsaidia mke wangu na mmoja wa wale vijana akimsaidia binti yule wa hakimu, tukawa tunakwenda huku tukipumzika hapa na pale Sauda kituongoza njia kuelekea ulipokuwa mlango wa kutokea Muifufu, muda nao ulikuwa ukiendelea kututupa mkono, kwa haraka haraka nilihisi tulikuwa tumebakiwa na dakika zisizozidi ishirini hivyo niazidi kuwahimiza japo safairi haikuwa nyepesi.

Hatimye tukafika mpaka eneo la tukio lakini cha ajabu ni kwamba mlango haukuwa wazi kama ambavyo tulidhani tungeukuta. “mmh! Mbona mlango wenyewe hauko wazi?” aliuliza Sauda ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wetu kwenye swala la mlango huo, mimi sikuona chochote zaidi ya eneo la pori kama yalivyo maeneo mengine. Ikanibidi kuwaelezea kila kitu kilivyokwenda nyumbani kwa Magugi na namna ambavyo nilifanikiwa kumlisha ule mkate na kumfanya afungue mlango, sote tukaamini kuwa tulikuwa tumechelewa kufika pale ndani ya saa moja na sasa Magugi alikuwa amerudiwa na akili zake na kuufunga mlango ule haraka kabla hatujafika. Sasa tufanya nini? Tutakwenda wapi ndani ya Muifufu Magugi asitupate na kutuua, tulikuwa tukijiuliza, sote tuliona kuwa mwisho wa maisha yetu ulikuwa umewadia.

Mara tukoana miili yetu ikinyanyuliwa juu na kuiacha aridhi, tukabaki tukielea hewani ingawa hakikuonekana kilichotunyanyua, kwa mbali tulisikia sauti za watu wakisogea eneo lile, tukakimbia na kujifucha kwenye vichaka lakini sauti uti za watu wale ziliendelea kutufuata kila upande ambao tulielekea, nikatoa yale mafuta aliyonipa Mnaro nikampaka mke wangu kisha nikajpaka mimi na kuwapa wengine wote wajipake, Mnaro linimbia mtu akipaka mafuta yale hawezi kuonwa hata na wachawi, labda mchawi mwenye uwezo mkubwa sana, hivyo niliamua kujaribu na nadhani tulifanikiwa maana watu wale walipita kwa kasi wakituvuka palepale tulipokuwa na hawakuonekana kutuona, tukaendela kuulizana nini kifanyike baada ya kuwa lile limetukosa. Ghafla tukaona miili yetu ikinyanyuliwa juu na kuiacha aridhi, tukawa tunaelea hewani kama vile hatukuwa na uzito wowote, kwa mbali ikasikika cheko kubwa ikisogea tulipo, na ilisikika kama cheko ya mwanamke, miili yetu ikiendelea kuelea hewani ilitolewa kwenye kichaka tulichokuwa tumejificha na kwenda kusimama mbele ya mwanamke mrefu sana aliyekuwa na nywele ndefu mpaka zinaburuza chini, mwanamke yule alionekana mrembo lakini hakuwa na mcho, hakuwa hata na mashimo ya mcho. Mwanamke huyu alikuwa akiifanya miili yetu atakavyo kwa mikono yake, aliweza kutupeleka juu, chini mbele, nyuma na hata pembeni bila kutugusa.

itaendelea sehemu ya 51


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here