SHARE

Mara kikaonekana kichwa cha Magugi kikielea hewani kama kiliundwa kwa moshi kikiongea, “hakuna hata mmoja kati yenu mwenye akili kunizidi, Sauda nilikuona kama ni msaliti wala sikukosea kukuhukumu kifo, wewe mzee Mikausho ukaleta hila zako za kudai Sauda hakuwa na hatia lakini nilikuona kama unaongopa, na niliona chote ulichokifanya, bado haikutosha ukaamua kumuua mtumishi wangu muaminifu na kuniletea muuaji, hivi mlidhani mimi ni mjinga kiasi hicho?” alihoji Magugi ambaye alionekana kuzijua hila zetu mapema tu.

“Dawa zako hazina nguvu mbele yangu kijana, na mwisho wako umefika, na kama ulitaka kuuju ufunguo wa mlango wa Muifufu leo umekutana nao, huu ndo ufunguo wangu na leo utaitoa roho yako” alisema Magugi akinionesha yule mwnamke ambaye alikuwa ametuteka. “Tunu endelea na kazi yako, nataka Sauda na mzee Mikausho watangulie kufa kisha wengine wafuate maana wao ndio viongozi wa usaliti huu” kilisema kichwa kile cha Magugi kisha kikatoweka. Hofu ilitawala sana, kila mtu alikuwa akiongea neno lake kujaribu kumsihi mwanamke yule asiye na macho asituue, mwanamke yule alionekana kuwa na hisia za hali ya juu kwani aliweza kujua kila kitu kilipo bila kuona, pengine angekuwa anategemea macho asingetuona kama wale waliotupita baada ya kujipaka yale mafuta. Tunu akanyanyua mkono wake juu sana na mwili wa Sauda ukafuata mkono ule kwa kuinuka juu sana kisha akafanya kama kamrusha na mwili wake ukapigizwa kwenye miti kwa kasi kubwa na Sauda akatua chini kama mzoga,na kutuli tulii! alionekana kama viungo vingi vya mwili wake vilikuwa vimevunjika, ikafuata zamu ya mzee Mikausho ambaye naye kilimkuta kama kilicho mkuta Sauda, hofu ikatanda, hakuna aliyejua nani atafuata!.

Ilikuwa ni zamu ya Hisham, akapigizwa kwenye miti huko naye akatua chini na kutulia. Nikapata wazo la ghafla na kutoa lile yai la bundi ambalo lilikuwa limebaki kwenye mkoba na kumuonesha yule mwanamke.”kama ukituruhusu kuondoka nitakupa yai hili”nilisema na mwanamke yule akasita kuendelea na zoezi lake,akawa kama anasikilizia kujua nilikuwa namuonesha nini maana hakuwa na macho, alikuwa anatumia hisia tu. “tufungulie mlango tuondoke kisha nakupa” nilimwambia mwanamke yule ambaye alionekana kuvutiwa na nilichokuwa nimekishika. “niwaachie wangapi?” alianza kujadili biashara mwanamke yule. “sote tuliobakia, nilisema kwa kujiamini” lakini mwanamke yule akawausha mbali vijana wale watatu, wakajigonga kwenye miti kama ilivyokuwa kwa Sauda, mzee Mikausho na Hisham.

Sasa nilikuwa nimebaki na mke wangu na yule binti wa hakimu tu. “kwa yai hilo moja naweza kuwaachia ninyi watatu tu” alisema mwanamke yule huku akitutua chini polepole kabisa. Nilisikitika sana kuwapoteza wote ambao tulikuwa tumepambana pamoja kwenye harakati za kutoroka Muifufu lakini sikuwa na namna. Ikanibidi kuikubali hofa ile ya sisi watatu, “nipe hilo yai haraka, hatuna muda” alisema yule mwanamke kwa sauti ya kuamisha, nikaingiwa na mashaka kidigo, itakuwaje kama nitampa anachokitaka kisha akaendela na zoezi la kutuua? Niijiuliza. “tutajuaje kam kweli tukikupa yai hili utatuachia tuondoke?” nilimuuliza kuonesha wasiwasi wangu.

Yule mwanamke kabaki kimya, hakutoa jibu lolote ndani ya sekunde kama 20, kisha akazungumza “mnanichelewesha” ilikuwa ni kama hakusikia swali langu. Nikafikiri kwa kina na kuona sikuwa na chaguo lingine, nikaamua kumuamini mwanamke yule na kumkabidhi lile yai.

Usikose sehemu ya 52


1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here