SHARE

Mahakama moja nchini Misri jana Jumamosi imemtia hatiani rais wazamani wa Misri Mohammed Morsi na watu wengine 19 kwa kosa la kuikashifu mahakama.

Kutokana na kosa hilo mahakama imewahukumu kwenda jela miaka mitatu katika hukumu hiyo iliyotangazwa moja kwa moja kupitia Televisheni.

Kesi hiyo ilikuwa ikiwahusisha washitakiwa 25 ambapo watano miongoni mwao ikiwa ni pamoja na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu Alaa Abdel- Fattah na mchambuzi wa masuala ya kisiasa Amr Hamzawy walitozwa faini ya paundi za Misri 30,000 kila mmoja.

Abdel-Fattah anatumikia kifungo cha miaka mitano kwa kushiriki maandamano ambayo hayakuwa na kibali kisheria mwaka 2013. Washitakiwa wote wanadaiwa kuikashifu mahakama kwa kutoa kauli ambazo zilitangazwa ama kupitia Televisheni, radio, mitandao ya kijamiii au katika machapisho ambayo mahakama imeona ni uchochezi.

Credit – DW


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here