SHARE

YULE straika wa Mbao FC, Habibu Kiyombo, aliyewafanyia Yanga kitu mbaya katika mechi yao ya Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba amesema , anatamani awe mchezaji bora wa muda wote kama walivyo wakali Muargentina Lionel Messi na Mreno Christian Ronaldo.

Kiyombo ambaye ndiye aliyewafunga Yanga mabao yote mawili juzi Jumapili walipocheza mchezo wa ligi kuu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

“Niliwahi kuwafunga bao moja kwenye mechi yetu ya mwisho ya ligi kuu, kwa hiyo hata jana Jumapili, nilitamani kuwafunga, jambo ambalo nimelitekeleza. Nawashukuru wachezaji na kocha wetu ( Mrundi Ettiene Ndayiragije) kwa kukamilisha malengo yetu,”amesema Kiyombo.

“Natamani kuwa mchezaji bora wa muda wote, mfungaji bora na timu yangu ili iwe nafasi nzuri kama wanavyofanya Messi na Ronaldo kule kwao, natamani sana hivyo nitazidi kupambana hadi nifanikiwe.”

Mshambuliaji huyo ambaye tayari amefunga mabao 12, ambayo ni pamoja na ya FA na ligi kuu amesema, bado ushindani ni mkali kwa nyota wengine wanaopambana kusaka kiatu cha mfungaji bora hivyo hatakata tamaa hadi mwisho wa Ligi.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here