SHARE

USHINDI wa mabao 2-0 walioupata Azam dhidi ya Mwenge FC katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi, umempa jeuri kocha wa timu hiyo, Iddi Cheche.

Azam ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo, waliibuka na ushindi huo katika mchezo uliochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.

Akizungumzia matokeo hayo, Cheche alisema atahakikisha wanashinda kila mchezo ili waweze kutetea ubingwa wao walioupata msimu uliopita baada ya kuifunga bao 1-0 Simba katika mchezo wa fainali uliochezwa Amaan.

Cheche alisema wamejipanga vizuri na hawatatoa nafasi kwa wapinzani wao kushinda kirahisi, kwani kila mchezo kwao ni fainali.

Alisema haikuwa rahisi kwao kushinda dhidi ya Mwenge FC, kwa kuwa mchezo ulikuwa mgumu, lakini vijana wake walipigana na kuondoka na pointi.
“Sisi kama mabingwa watetezi, tunahitaji kulitetea kombe letu msimu huu,” alisema Cheche.

Kwa upande wa kocha wa Mwenge FC, Salum Ali Salum, alisema walifungwa mchezo huo kutokana na vijana wake kukosa uzoefu.

Salum alisema mchezo ulikuwa mzuri, kwani wachezaji wake walicheza inavyotakiwa, lakini haikuwa bahati yao kushinda.

Alisema amefanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mchezo wao dhidi ya Azam ili waweze kuibuka na ushindi dhidi ya Simba.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here