SHARE

SIRI ya kichapo cha mabao 2-0 waliyofungwa Yanga dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita, imefichuka.

Huo ni mchezo wa tatu mfululizo Yanga kupoteza katika Uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Mbao FC ambayo ilipanda daraja msimu uliopita.

Kwa mara ya kwanza Yanga walifungwa bao 1-0 na Mbao FC kwenye uwanja huo wa Kirumba katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Tanzania ‘Azam Confederation Cup’, kisha kubamizwa tena bao 1-0 kwenye mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu msimu uliopita.

Kwenye mchezo wa juzi ambao ndio wa tatu, Yanga walipokea kichapo hicho cha mabao 2-0 tofauti na mechi zilizopita na kuzua maneno kwa mashabiki na wadau wa soka.

Mmoja wa wadau hao wa soka ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Mbuyu Twite, ambaye alifichua kwamba kipigo hicho kinatokana na benchi linaloongozwa na kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa, pamoja Noel Mwandila kushindwa kupanga kikosi hicho vizuri.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here