SHARE

KOCHA wa Simba, Masoud Djuma, amemkingia kifua mshambuliaji wake, Juma Luizio, akidai kuwa ataendelea kumpa nafasi ndani ya kikosi hicho kwa kuwa ni mchezaji wa timu hiyo.

Ametoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya wapenzi wa timu hiyo kudai kuwa mchezaji huyo amekuwa akiaminiwa na makocha na kupewa nafasi lakini haonyeshi kiwango kizuri.

Djuma alisema kwa sasa katika kikosi chake kuna mastraika wawili ambao ni Luizio na John Bocco, hivyo ni lazima mmoja wao apate muda wa kupumzika na mwingine acheze.

Alisema anachoangalia kwa sasa ni kuhakikisha kila mchezaji anapata nafasi ya kucheza na kuonyesha uwezo wake, kwani asipofanya hivyo lazima watalalamika.

“Luizio ni mchezaji wa Simba hivyo lazima acheze, lakini pia Bocco anahitaji muda wa kupumzika kwa sababu hawezi kucheza mfululizo.

“Hao wanaosema anapewa nafasi na haonyeshi kiwango je, akikaa benchi watakuja kulaumu na kuuliza mbona mchezaji fulani achezeshwi?” alihoji Djuma.

Kocha huyo raia wa Burundi, aliongeza kuwa Simba inakabiliwa na mashindano mengi ikiwamo Kombe la Mapinduzi, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho barani Afrika, hivyo anahitaji kupima uwezo wa kila mchezaji.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here