SHARE

IMEFICHUKA kuwa straika wa Mbao FC, Habib Kiyombo aliyewatungua Yanga mabao mawili peke yake wikiendi iliyopita, ni zao la timu ya vijana ya Simba.

Kiyombo ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika mashindano yote msimu huu, akiwa amefunga mara 12, ambapo saba kati ya hayo amefunga Ligi Kuu ikiwemo hayo mawili aliyowafunga Yanga.

Sasa kumbe straika huyo aliyeitungua pia Simba bao moja katika sare ya 2-2 dhidi ya Mbao FC msimu huu, ametokea Msimbazi.

Kiyombo alisajiliwa na Mbao FC msimu uliopita wakati wa dirisha dogo la usajili akitokea Lipuli iliyokuwa Ligi Daraja la Kwanza kwa wakati huo.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Kiyombo alisema kuwa “Nilikwenda Simba B kufanya majaribio na nikafuzu chini ya kocha Nico Kiondo, hiyo ilikuwa mwaka juzi .

Hata hivyo sikukaa sana Simba ndipo nikapata timu nyingine ya Lipuli.

“Nilijiunga na Lipuli kwasababu lengo langu ni kupiga hatua kisoka na ndiyo maana juhudi zangu zimenifikisha hapa nilipo na ninacheza mechi za Ligi Kuu na msimu huu nimezifunga Simba na Yanga, ni faraja kwangu,” alisema Kiyombo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here