SHARE

Droo ya raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) inachezeshwa kesho Januari 5, 2018 ikishirikisha timu 32.

Raundi hiyo ya tatu itahusisha timu nne za mabingwa wa mikoa, tatu za Ligi Daraja la Pili, 12 za Ligi Daraja la Kwanza na 13 za Ligi Kuu.

Hatua hiyo ya raundi ya tatu inabakiza timu 16, zitakazopambana kwenye hatua inayofuata.

Timu za Ligi Kuu zilioingia hatua hiyo ya raundi ya tatu ni Azam FC, Yanga, Mtibwa Sugar, Mbao FC, Majimaji, Kagera Sugar, Mwadui, Stand United, Ruvu Shooting, Njombe Mji, Singida United, Ndanda ya Mtwara na Tanzania Prisons.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here