SHARE

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewasaidia wasanii Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa kuwapeleka studio ili waweze kurudi rasmi katika kazi yao ya muziki.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amesema kuwa leo Januari 5, 2018 amefanikiwa kuwafikisha wasanii hao katika studio za Wanene ambapo hapo wataweza kurekodiwa kazi zao na kusaidiwa mambo mengi kama ambavyo ameweza kuongea na Mkurugenzi wa studio hizo.

“Tunajua kwamba hawa watu hawakuwa kwenye ulimwengu huu wa muziki muda hivyo wanahitaji ‘support’ kwani mtu anaporudi vitu vingi vinakuwa vipya hivyo nikaona ni vyeme kukutana nao na wamenieleza mpango wao ni kurudi kwenye tasnia ya muziki. Mimi kama Naibu Waziri nikaona ni vyema niwachukue na kuwaleta hapa studio za Wanene kwani tayari niliongea na Mkurugenzi wa studio hizi na aliahidi yupo tayari kuwasaidia kwa hali na mali” alisema Shonza

Aidha kwa upande wake Babu Seya ameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa yote na kusema yeye sasa anachotaraji ni kufanya kazi tu na kusema kuwa mambo makubwa yatakuja mbele.

Babu Seya na Papii Kocha waliachiwa huru kwa msahama wa Rais Magufuli mnamo Disemba 9, 2017 na walitoka gerezani siku hiyo hiyo baada ya hapo walipumzika kwa wiki tatu na kuja kukutana na Rais Magufuli Ikulu Januari 2, 2018 ambapo walikwenda kumshukuru.

Babu Seya na Papii Kocha wametumikia kifungo kwa miaka 13 jela kufuatia kukutwa na hatia ya kubaka na kulawiti watoto wadogo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here