SHARE

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog yupo kwenye mapumziko kwao Cameroon amesema, yuko tayari kuifundisha Yanga na atawapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Omog ambaye katika mapumziko yake hayo amejipa mwezi mmoja na baada ya hapo, atarudi mzigoni kufundisha.

Kocha huyo mpole, amejipa majukumu hayo baada ya Simba kumvunjia mkataba wa kuinoa timu hiyo ya Msimbazi na uongozi ukampa majukumu yote, Mrundi Masoud Djumba.

“Nimeamua kupumzika, ni kipindi kirefu kimepita sijakaa na familia yangu, nimejipa muda wa mwezi mmoja ili akili yangu itulie na baada ya hapo nitakuwa tayari kuifundisha timu yoyote itakayo nihitaji,”amesema Omog.

Akizungumzia Yanga kama anaweza kuifundisha, Omog amesema: “Kila kitu kinawezekana, naweza kuifundisha Yanga , lakini ni kwa hapo baadaye baada ya kumaliza mapumziko yangu niliyojipa.”

Omog ndiyo kocha pekee aliyeipa ubingwa klabu tajiri ya Azam FC msimu wa mwaka 2012-2013, ameachana na Simba ikiwa inaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here