SHARE

EMMANUEL Okwi bado ni pasua kichwa, jambo linawaweka juu mashabiki wa klabu hiyo, lakini namna John Bocco ‘Adebayor’ alivyofanikiwa kuishika Msimbazi, ni kiasi cha kuhesabu siku tu kabla ya kumpoteza kabisa raia huyo kutoka Uganda.

Ni hivi. Bocco amezidi kuwa moto ndani ya Simba na kwa sasa anahitaji kufunga mabao mawili tu, ili kumfikia kinara wa mabao klabuni hapo, yaani Okwi aliyeanza msimu kwa kasi ya ajabu kabla ya kuzimika ghafla.

Awali, Bocco alifunikwa na uwepo wa Okwi katika kikosi cha Simba kwani wakati wakicheza pamoja alifunga bao moja tu katika mechi tisa, lakini sasa mambo yamegeuka.

Habari njema kwa Bocco ni kwamba tangu Okwi alipoumia Novemba mwaka jana, ameibeba Simba na kufunga mabao matano katika mechi sita tu.

Bocco alianza kasi yake ya mabao kwenye mechi dhidi ya Prisons ambayo ilikuwa ya kwanza kwa Okwi kuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu. Bocco aliipa Simba ushindi wa bao 1-0.

Kama hiyo haitoshi, nahodha huyo wa zamani wa Azam akafunga bao jingine dhidi ya Green Warriors kwenye kombe la FA lakini timu yake ikapoteza kwa mikwaju ya penalti na kutolewa.

Bocco alifunga mabao mengine mawili kwenye mechi dhidi ya Ndanda ambapo Simba ilishinda 2-0 kabla ya kufunga jingine moja kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Pemba.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here