SHARE

Klabu ya soka ya URA imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Mapinduzi baada ya kuitoa Yanga SC kwa mikwaju ya Penalti kwenye uwanja wa Amaan jioni hii.

Timu hizo mbili zilimaliza dakika 90 za nusu fainali ya kwanza bila kufungana hivyo kuingia kwenye changamoto ya mikwaju ya Penalti ambapo timu zote zilianza vizuri hadi Penalti ya tano ambapo mshambuliaji Obrey Chirwa alikosa.

URA imefanikiwa kuziondoa timu za Simba na Yanga katika michuano hiyo. Ilianza kwa kuifunga Simba kwenye mchezo wa mwisho wa kuamua nani aende nusu fainali kutoka kundi B ambapo ilishinda bao 1-0.

Timu hiyo kutoka Mamlaka ya kukusanya mapato nchini Uganda sasa itasubiri kujua itakutana na nani kwenye mchezo wa fainali baada ya mchezo wa usiku utakaowakutanisha Azam FC na Singida United.

Azam FC na Singida United zinacheza majira ya saa 2:00 usiku kwenye nusu fainali ya pili ambapo mshindi atakutana na URA katika fainali siku ya jumamosi Januari 13.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here