SHARE

Na Jerry C. Muro
Dar es Salaam, Tanzania
09/01/2018

Leo(jana) Dunia, Afrika na Tanzania Imeshuhudia Historia ingine ya Hatua Muhimu ya Kisiasa kufuatia hatua ya Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kukubali kukutana na Aliyekuwa Mgombea wa Nafasi ya Urais kupitia “Muungano ” wa Baadhi ya vyama vya Upinzani nchini UKAWA Ndugu Mhe Edward Lowassa waliokutana katika Ikulu ya Dar es Salaam, na kisha Wote kwa pamoja kuzungumza na Waandishi wa Habari.

Kwetu hii Imekuwa Hatua kubwa sana ya Kuendelea kuongeza Upendo, umoja na mshikamano wa Kisiasa nchini Tanzania , yapo mengi wameongea na kukubaliana lakini kubwa kwangu ni kuwaona wametoka pamoja kwa Tabasamu na Kushikana Mikono ikiwa ni Ishira ya Maelewano.

Nimeshangazwa sana na tweet ya Godbless Lema ya kumlaumu Edward Lowassa kwa kauli ya kumpongeza Rais Magufuli mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Dar es Salaam.

Lema hakupenda kauli zile na anataka asitokee wa kumpongeza Rais Magufuli kwa sababu ya matukio ya kushambuliwa Lissu, kuokotwa miili ufukweni, uchumi unashuka, benki zinafungwa na mkwe wa Lowassa aliyopo gerezani.

Ukiangalia watu wenye nia njema na nchi na ambao waliamini kuwa nchi imepasuka na inahitaji kuunganishwa na wanasiasa walikuwa wanatamani sana kuona Mhe. Lowassa akiweka dhamira yake kwanza kwa sababu ndiye mgombea aliyepata kura nyingi baada ya Mhe. Magufuli katika uchaguzi mkuu 2015.

Wapenda nchi hii walipoona Lowassa na Magufuli wanashikana mikono na wanapongezana kwa uongozi mzuri wamefurahi kuwa hii ni hatua muhimu ya kuliunganisha Taifa.

Nimeshangaa sana kumsoma Godbless Lema akilaumu kauli ya Mhe Lowass . Imenithibitishia kuwa huyu mtu anapenda kuona Taifa likiendelea kugawanyika. Anapenda kuona chechee, na ndio maana amekuwa akitaka siasa za mapambano.

Lema ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA , ni mbunge na mtu mwenye ushawishi ndani ya CHADEMA . Kwa tunaomjua ni rafiki mkubwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe, Lema anajiona ni mwenye Chama kama Mbowe. Kwa hiyo kauli yake hii bila shaka ndio msimamo wa mwenyekiti wake na rafiki yake Mhe. Mbowe.

Ndio kusema CHADEMA wamechukizwa sana na kauli ya Mjumbe wa Kamati Kuu yao Mhe. Edward Lowassa. Ndio kusema CHADEMA haipendi kuona taifa linaungana.

Hadi hapo ni muhimu kukubali kuwa kumbe mtaji wa CHADEMA ni taifa lililogawanyika, lililojaa chechee na fitina.

Sasa naanza kuelewa kwa nini viongozi wanakimbia CHADEMA, naamini kauli za Rais Magufuli kwamba wapo wengi wanaomba kurudi CCM.

Huko tulikotoka tuliambiwa CCM wananunua viongozi wa CHADEMA sasa leo tumeshuhudia viongozi wakubwa wenye pesa zao. Najiuliza hivi Lowassa nae kanunuliwa ili akutane na Magufuli? Najiuliza kalipwa hela ili aseme aliyayosema? Bahati nzuri Magufuli mwenyewe anasema Lowassa kaomba mara nyingi kukutana na Mhe. Rais Magufuli na leo kaona amkubalie.

Kwingineko Muslim Hassanali mmoja ya watu muhimu ndani ya CHADEMA mwenye siri zote za fedha na aliyekuwa kiongozi katika baraza la wadhamini ameondoka na kujiunga CCM . Tunaofuatilia siasa za CHADEMA tunajua kuna msululu wa viongozi wabunge na madiwani wameomba kurudi CCM, sasa najiuliza huyu bundi aliyetua CHADEMA ni bundi wa namna gani?

Kama kweli tunahitaji upinzani nadhani tunapaswa kufanya kitu. CHADEM inaondoka, ilianzisha yenyewe kumchukua Nyalandu na sasa hizi ndio gharama zake. Ilisahau kuwa ugomvi wa mawe hauanzishwi ukiwa unaishi kwenye nyumba ya vioo.

Wasalamu
Jerry C. Muro


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here