SHARE
Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikatiakitembelea maeneo ya Hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila alipotyembelera hospitali hiyo ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam.. wa kwanza kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali hiyo Prof. Aboud Said.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ameagiza wagonjwa wasiotakiwa kufanyiwa upasuaji waliopo hospitali ya taifa Muhimbili kuhamishiwa hospitali ya Mloganzila.

Waziri Ummy ametoa agizo leo alipotembelea hospitali ya Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Kampasi ya  Mloganzila Jijini Dar es Salaam. Ameeleza lengo kuu la kuhamishwa kwa wagonjwa hao ni kupunguza msongamano katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ummy ameongeza kuwa Wizara yake imejipanga kuongeza madaktari bingwa kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda kuwahudumia wagonjwa watakao hamishiwa katika hospitali ya Mloganzila. Pia amezitaka hospitali za Wilaya kama Amana na Mwananyamala kuwapa rufaa wagonjwa wasiohitaji upasuaji ya kwenda Mloganzila.

Kwa Upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila, Professa Said Abood, amesema kuwa wamejipanga kuhudumia wagonjwa wote watakao wasili kutoka Muhimbili.

Profesa Abood ametaja Magonjwa yaliyoagizwa kutibiwa hospitalini hapo kuwa ni yale yasiyo hitaji upasuaji kitaalamu yanaitwa Magonjwa ya ndani kama vile Malaria, na mengine. Aidha Abood amesema tayari wameshaanza kuwapokea wagonjwa hao wanaotoka Muhimbili.

Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na waandishi wa habari alipotyembelea hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam,wa kwanza kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali hiyo prof. Aboud Said.
Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wananchi waliokuwa wanasuburi huduma kwenye hospitali ya taaluma na Tiba Mloganzila wakati alipotyembelera hospitali hiyo ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam.. wa kwanza kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali hiyo Prof. Aboud Said.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here