SHARE

Baraza la Vijana Chama  cha Demokrasia na Maendeleo Taifa  (BAVICHA) umeuomba uongozi wa serikali kutoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizotolewa na Tundu Lissu  kuhusu mwenendo mzima wa utendaji.

Katibu Mkuu (BAVICHA) Taifa, Julias Mwita akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam katika ofisi za makao makuu ya Chadema.

Pia, Bavicha imesema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka hana hoja wala uwezo wa kujibu masuala anayozungumza Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema.

Msimamo huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita akizungumza na waandishi wa habari akijibu  kauli ya Shaka ya  kuwa alichofanya Lissu ni kujitafutia umaarufu na  kuikosanisha Tanzania na Kenya.

“Shaka alichofanya ni cha upotoshaji kwa watanzania, na hafai kuzungumzia hilo kwani yeye ni kiongozi mdogo tu, tunamtaka  aliyemtuma ambaye ni rais Magufuli atoke na ajibu yeye,” amesema Mwita.

Amesema  walitegemea Shaka angetoka hadharani na kuishinikiza serikali imtibu Lissu na atoe takwimu za ajira kwa vijana zilizotolewa na serikali.

Pia amesema walitegemea kama siyo serikali iliyotekeleza shambulizi dhidi ya Lissu, angesema hadi sasa ni watuhumiwa wangapi wamekamatwa.

Amesema kwa kauli za Naibu Katibu huyo wa UVCCM zimewachukiza kwa kuwa amejaribu kulihadaa taifa kwa kuzungumza mambo asiyoyajua na kwamba amepotoshwa na waliomtuma kwa makusudi.

Amekumbusha kuwa Lissu hakusema yeye ndiye mwanasiasa wa kwanza kushambuliwa kwa risasi ila ni mwanasiasa wa kwanza wa upinzani kushambuliwa kwa risasi.

Hivi karibuni Lissu akiwa nchini Kenya alisema serikali ya rais Magufuli ndiyo inayohusika na shambulizi dhidi yake.

Pia serikali imeshindwa kugharamia matibabu na kulilaumu Bunge kushindwa kumuhudumia kwa kuwa ni haki yake kama  Mbunge wa Singida  Mashariki.

Kwa sasa Lissu yupo nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu ya viungo kufuatia Septemba 7, 2017 mjini Dodoma kupigwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa akishiriki vikao vya Bunge. Alilazwa  katika hospitali moja Nairobi nchini Kenya kwa takribani miezi minne


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here