SHARE

YANGA imeyaaga mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Kisiwani Zanzibar baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 5-4 na URA ya Uganda.

Yanga ambayo imeifuata Simba kurudi nyumbani Tanzania Bara ni baada ya kumaliza dakika 90 kwa suluhu ya bila kufungana.

Mzambia Obrey Chirwa ambaye ameungana na timu jana asubuhi na akaaminiwa kupewa nafasi ya kucheza kuanzia dakika ya 53 akichukua nafasi ya Pius Buswita, ndiye aliyekosa penalti hiyo, iliyowaondoa Yanga katika mashindano hayo hatua ya nusu fainali.

Yanga walipiga penalti nne wakapata kupitia kwa Papy Tshishimbi, Hassan Ramadhan ‘Kessy’, Raphael Daud na Gadiel Michael kabla ya hiyo ya tano aliyomalizia, Chirwa akakosa.

Kwa matokeo hayo, Yanga wataanza safari ya kurudi Dar es Salaam na boti ya asubuhi na URA wanasubiri mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Azam FC na Singida United itakayochezwa saa 02:15, usiku wa leo Jumatano.

Hatika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, kiungo wa Yanga, Said Juma ‘Makapu’ alichaguliwa kuwa mchezaji bora ‘Man Of The Match).

Makapu amesema: “Sababu ya kufanya vizuri ni kujituma, lengo lilikuwa ni kuonyesha kipaji changu kwa Wazanzibari wenzangu na Watanzania wote, wajue kumbe naweza na pia nahitaji nafasi zaidi ya kucheza.”

Akizungumzia mchezo huo, Makapu anasema, ulikuwa mgumu na wapinzani wao walikuwa wazuri zaidi kwenye safu ya ulinzi, ndiyo maana wakashindwa kufunga na walipokwenda kwenda kwenye penalti ndiyo ikawa hivyo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here