SHARE

Serikali nchini Ugiriki imeikamata meli yenye usajili wa Tanzania, eneo la Crete nchini humo jana Jumatano, ikiwa na shehena ya kutengeneza silaha za milipuko

Shehena hiyo ilichukuliwa nchini Uturuki, na ilikuwa ikipelekwa Misrata, Libya.

Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa uliweka vikwazo vinavyozuia kuuza, kupeleka au kusambaza silaha Libya tangu mwaka 2011

Nyaraka zilizkuwa kwenye meli hiyo zilionyesha mzigo huo ulipakiwa kwenye bandari za Uturuki za Mersin na Iskenderum na safari yake ilikuwa iishie Djibouti na Oman.

Lakini walinzi wa eneo la bahari wakisema uchunguzi wa awali umeonyesha nahodha wa meli hiyo alikuwa ameagizwa na wamiliki wa meli hiyo kwenda mji wa Misrata kupeleka na kupakuwa mzigo wote

Ramani za kwenda Djibout na Oman hazikukutwa kwenye kitabu cha meli hiyo

Watu nane waliokuwepo kwenye meli hiyo wamekamatwa na watapelekwa mahakamani leo Alhamisi


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here