SHARE

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema Mapinduzi ya mwaka 1964 ndiyo yaliyoleta ukombozi Zanzibar na yeyote anayabeza atafute mahali pa kwenda.

Dk. Shein aliyasema hayo katika ufunguzi wa soko la Kinyasini, Mkoa wa Kaskazini, Unguja ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema, Mapinduzi hayo yameongeza fursa kwa wananchi ambao wote wamefaidika na hakuna mwananchi wa Zanzibar ambaye hajafaidika.

Dk. Shein alisema tangu awamu ya kwanza hadi sasa, awamu zote zinaendelea kuyaenzi, kuyatunza na kuyalinda Mapinduzi na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.

Alisisitiza kuwa soko hilo ni la wananchi wote wa Kaskazini A na B kwa maisha yao pamoja na wananchi wengine wa mikoa mengine ambao watakwenda kufuata mahitaji sokoni hapo. Dk. Shein aliongeza kuwa si vyema soko hilo likageuzwa sehemu ya kupiga siasa na kuwataka wananchi kulitumia vyema soko hilo, ili waweze kupata tija.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here