SHARE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohamed Shein amesema serikali yake itaendelea kuimarisha umoja, mshimakano, na maendeleo katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo kuna umuhimu ya kuenziwa kwa mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Dokta Ali Mohamed Shein ameyasema hayo leo katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibaambapo amesema ili kufanikisha kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda mwaka serikali yake itaendelea kusimamia kwa karibu sekta ya kilimo.

“Ninapongeza juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. John Pombe Magufuli za kupambana na vitendo vya ufisadi, rushwa, vita dhidi ya dawa za kulevya na juhudi za kulinda rasilimali za taifa kwa vitendo ikiwemo rasilimali madini”amesema Dkt Shein

Katika sherehe hizo za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar wamehudhuria viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais Dokta John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa, Rais mstaafu wa awamu wa nne Dokta Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa awamu ya pili Al Haji Hassani Mwinyi na viongozi wengine wa chama na serikali


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here