SHARE

Muda wote huu mke wangu alikuwa amelala, hakushtuka hata kidogo pamoja na Mnaro kuongea kwa sauti kubwa sana, hata zile vurugu zake za maupepo hazikusumbua usingizi wake, nadhani ulikuwa ni uchawi wa Mnaro kutaka mimi tu ndo nisikie maongezi yake ndio maana alingoja mpaka mke wangu alale ndio aje.

Asubuhi tuliamka mida ya saa tatu, mke wangu alitangulia kuamka kisha kaniamsha haraka baada ya kushangazwa na hali ya chumba kwani wakati analala chumba kilikuwa katika mpangilio wake, hakukuwa na namna ikanibidi kumthimulia yaliyojili baada ya kupotea kwake, nikamuelezea msaada ambao alinipa Mnaro mpaka kufanikisha zoezi lile pamoja na mkataba wetu wa kuhakikisha namejeshea Sauda katika maisha yake, kisha nikamuelezea ujio wa Mnaro usiku na malalamiko aliyokujanayo. “mmh! Kurudi tena Muifufu ni kwenda kufa, usithubutu” alisema mke wangu baada ya maelezo yangu marefu. “nilimueleza waziwazi Mnaro kuwa siko tayari kurudi Muifufu lakini cha ajabu alisema ni lazima nitarudi na akanitaka kumtafuta nikimuhitaji, yani ni kama ana uhakika kuwa mimi nitataka kurudi huko” nilieza. “huyu atatusumbua sana, unaonaje tukiama hii nyumba?” mke wangu alitoa ushauri wake ambao ulionesha waziwazi kuwa maelezo yangu hayakutosheleza kumuonesha Mnaro alikuwa na nguvu kiasi gani. “hatuwezi kumkimbia mke wangu, akitutaka atatufuata popote tutakapokuwepo” nilijaribu kumuelewesha mke wangu ambaye ainielewa. “ila cha msingi ni kuwa tuko pamoja na sitoruhusu tena tutengane” nilijaribu kumfariji.

Tukaendelea na maisha yetu kama kawaida lakini watu walikuwa wanatushangaa sana tulipokuwa tukipita mitaani tukiwa tumeongozana kama ambavyo tulikuwa tumezoea kufanya, nadhani hii ilitokana na watu hawa kujua kuwa mke wangu alikuwa amepotea, walikuwa wakishangaa kaudije wakati watu wengi sana kwenye eneo lile walikwishaga potea na hawakuwahi kurudi. Wakati mwingine watu walitusimamisha na kujaribu kuhoji maswali mbalimbali lakini hatukuwa tukipenda kuliongelea swala lili.

Siku kama ya nne toka tulipotoroka Muifufu alitujia nyumbani mzee wa kama miaka 70 akiwa na mkewe na wakatuelezea juu ya kupotea kwa binti yao miaka saba iliyopita, mazingira ya kupotea kwake yalifanana sana na yale ya kupotea kwa mke wangu, wazee wale wakataka kujua namna gani nilimpata mke wangu ili na wao waweze kuitumia njia hiyo kumpata binti yao. “mzee maneno yanayosemwa ni mengi lakini mengi sio ya kweli, mke wangu kweli alipotea lakini yeye alitekwa na mjambazi na walinipigia simu wakitaka pesa ili wamuachie hivyo nikatafuta pesa na kuwapa nao wakamuachia” nilidanganya ili kuwatoa njiani wazee wale. “kweli majambazi wanaweza kumteka mtu kisha wakamvua nguo na kuziacha?” alihoji mzee yule, swali ambalo kwakweli lilikuwa gumu. “ndio maana nikakwambia kuwa maneno yanayosemwa ni mengi ila mengi sio ya ukweli, sio kweli kama nguo za mke wangu zilibaki” nilijitetea na wazee wale wakakubali na kuondoka japo hawakuonesha kuniamini.

Maisha yetu yalianza kuwa magumu ghafla sana, sisi tulikuwa tunapeda maisha ya utulivu lakini sasa maisha yetu yalikuwa yanaangaliwa na kila mtu, wengine wakitutaka msaada ambao waliamini tunaweza kuwapa ila tulikuwa wachoyo wa kusaidia.

Mwisho tukafikia uamuzi wa kusafiri kidogo kwenda kuwaona wazazi wangu, mpaka tukirudi vuguvugu lile litakuwa limetulia.

Maisha nyumbani kwa wazazi wangu yalikuwa rahisi, hakukuwa na tabu kama ambazo tulizikimbia kule kwangu kwani huku hawakuwa wakijua juu ya janga ambalo liltukuta.

Maisha yakaendelea mpaka siku ambapo tulipanga safari mimi na mke wangu kwenda kumuona rafiki yangu Max ambaye nilikuwa sijaonana naye muda mrefu. Nakumbuka nilisikia kama muwasho fulani mgongoni nikawa najikuna huku najiandaa kwaajili ya safari yetu. Mara baada ya kuvaa fulana nyepesi ya ndani, kabla sijavaa shati mke wangu akashtushwa na alichokiona mgongoni mwangu “heee! Mbona kama una damu mgongoni?” aliuliza mke wangu huku akinisogelea na kuifunua fulana ile, akakutana na kidonda ambacho hakikujulikana kimetoka wapi, mke wangu akapatwa na wasiwasi mkubwa na akanisaidia na mimi kukiona kidonda kile kwa msaada wa kioo. Haraka sana nikakumbuka kuu ya kiapo changu kule mlima Kalingisi, niliahidiwa kupata jeraha mgongoni na jeraha hilo lisingepona mpaka nitakapotekeleza ahadi ya kumuua Magugi, pia nilipaswa kufanya haraka kwani niliambiwa kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo jeraha hilo linazidi kuwa kubwa na lingefikia hata kunitoa uhai. Japo jeraha lile halikuwa na maumivu, nilipatwa na wasiwasi mkubwa, maisha yangu yaikuwa yapo mashakani.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here