SHARE

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli anatarajia kumpokea Rais Paul Kagame wa Rwanda anaetaraji kuwasili Nchini Jumapili ya January 14 majira ya Asubuhi kwa Ziara ya Kikazi.

Akizungumza kuhusu ujio huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema uwezo mkubwa wa Rais Magufuli, Demokrasia imara na Amani ni miongoni mwa Mambo yanayowavutia Wageni kuja Tanzania akiwepo Rais Kagame wa Rwanda.

RC Makonda amesema baada ya Kuwasili kwa Rais Kagame kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere ataelekea moja kwa moja Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here