SHARE

Kalama Debos: Amekuwa mtu muhimu kwenye safu ya ushambuliaji ya URA, Debos anacheza nyuma ya mshambuliaji, ana uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi

Yahya Zayd: Nyota wa Azam, Yahya siyo mtu wa kupewa nafasi mara kwa mara kwani ni hatari akiwa na mpira kwenye eneo la adui, ana kasi na uwezo mkubwa wa kufunga kwa staili tofauti tofauti

Bokota Labama: Mabeki wa Azam wanabidi wamtolee macho straika huyu kwani ni mmoja wa nyota muhimu kwenye kikosi cha URA, Bokota ana jivunia nguvu na ufanisi mkubwa wa kucheza mipira ya hewani kutokana na kimo chake kirefu

Bernald Arthur: Raia huyu wa Ghana anayekipiga kwenye kikosi cha Azam siyo mtu wa kupewa nafasi nyingi ndani ya 18 kwani ana jicho la goli

Peter Lwasa: Katika mashindano ya msimu huu amepooza tofauti na miaka ya nyuma lakini ni mtu wa kupewa tahadhari kubwa kwani bado ni mmoja wa washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kufumania nyavu

Enock Atta: Ni winga ambaye amekuwa na mipango mikubwa katika klabu ya Azam, amekuwa ndiye mtu wa mipango ndani ya kikosi kwa kutengeneza nafasi nyingiza kufunga


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here