SHARE

Waziri Wa mambo ya ndani ya nchi DK mwigulu Nchemba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la iramba magharibi mkoa wa Singida amehaidi kumalizia mifuko 200 ya cement na na nondo 100 ili kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kata ya  kinampanda ambayo imekosekana kwa miaka mingi.

Waziri Nchemba amezungumza hayo baada ya kufika nakujiona hali ya kuridhisha ya ujenzi wa zahanati ya kata ya kinampanda ambao unafadhiliwa na ofisi ya mbunge wa jimbo akishirikiana na wananchi ambao wanachangia ujenzi huo.

“Kwa hatua ambayo mmeshafika hatuko mbali sana wiki ijayo nitashuhulikia tupate cement na nondo na nitaongea na mkandarasi na vijaana wengine wapenda maendeleo wawepo hapa ndani ya wiki mbili wawe wameshafika juu na tunapofika maliza mwaka wa fedha tuwe tushakamilisha ujenzi” alisema waziri Nchemba

Naye Diwani wa kata ya kinampanda  Justus Makala amesema kwasasa kinachohitajika kwa haraka katika ujenzi huo ni cement na nondo ili wapeleke jengo juu huku akisema wananchi wanajitolea kwa hali na mali kumsaidia mbunge kukamilisha zahanati hiyo mapema.

Mmoja ya wananchi Mathayo Kahaya ambaye alifika sehemu ya ujenzi amemshukuru mbunge kwa kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo huku akisema wananchi wanamwitikio mkubwa zaidi ya wakuchangia ujenzi huo iki wa kamalishe mapema.

Waziri Dkt.Mwigulu Nchemba yupo jimboni kwa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na ofisi ya mbunge akishirikiana na wananchi wa jimbo lake, miradi ambayo inaendelea kwasasa na ujenzi wa hosteli 22 za wasichana katika kata zote, zahanati na visima vya maji zaidi 75 vya kisasa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here