SHARE

Nilimwelezea mke wangu asili ya jeraha lile kwa kifupi, tukakubaliana kutafuta wataalamu wa tiba za asili (waganga) ili waweze kutusaidia. Wengi wa waganga hao walikuwa waongo, “hili jeraha limetokana na jini ambalo umetupiwa na jiani yako ambaye hapendi mafanikio yako”alisema mganga mmoja ambaye moja kwa moja tulimuona ni muongo na kupuuza maelekezo yake. Mganga mwingine akatuambia “kuna afiki yako ambaye mliwahi kugombana zamani sana lakini mkaja kupatana, mwenzio alibaki na kinyongo , akakuendea kwa mganga ukalogwa” huyu naye alikuwa muogo mwingine, tulihangaika sana kwa waganga wakati jeraha langu lilizidi kukua, sasa likaanza kuuma na kutoa harufu mbaya, lakini hatukukata tamaa ya kuhangaika, kila tulipoambiwa kuna mtaalamu mzuri sisi tulikwenda, tulikwenda mpaka kwenye maombi lakini hakukuwa na mafanikio

“inaonekana wewe uliwekeana kiapo na mtu kisha ukakivunja, na hii ni laana ya kiapo hicho” alisema mganga mmoja ambaye tulipelekwa na rafiki yangu kujaibu kama anaweza kutusaidia,mganga huyu nilimdharau mara tu baada ya kumuona kutokana na umri wake mdogo, mara nyingi waganga huwa wazee lakini huyu alikuwa kijana mdogo tu. “enhee, tunawezaje kulitibu hilo tatizo?” niliuliza kwa shauku baadaya kuona huyu mganga wa leo alikuwa wa kweli. “tiba pekee iliyopo ni kufanya ambacho uliapa kukifanya kisha ukamuombe msamaha huyo mliyeapizana kwa kujaribu kukiuka kiapo, kama akikusamehe basi utapoana. Nilijawa na simanzi baada ya maelezo hayo, kwani yalikuwa yakimanisha nirudi Muifufu, nikamuga mganga yule na kurrudi nyumbani kwa msaada wa rafiki yangu na baba ambaye tulikuwa tumeendanae kwa mganga yule.

“Jamani nimewahita hapa kwaajili ya kuongelea afya yangu” nilianza kuongea kwenye kikao ambacho niliwaita ndugu zangu na mke wangu. “ugonwa huu umetusumbua sana na naona unaleta umasikini nyumbani maana kila kinachopatikana kinatumika kutibia ugonjwa huu usiopona, sasa imetosha. Sote tunajua dawa ya ugonjwa huu nikurudi Muifufu, kwanini tunajidanganya na ukweli tunao? Sasa nimeamua kuwa nitarudi Muifufu kujaribu kupata tiba ya ugonjwa huu, kama nitakufa basi itakuwa mepangwa hivyo” nilimaliza maneno yale ambayo niliyatoa kwa uchungu sana, baadhi ya ndugu zangu hawakuweza kujizuia kutoa machozi baada ya maelezo yale, wengi walona ni kama walikwisha nipoteza. Afya yangu ilikuwa imedhohofu sana, nilikuwa nimekonda mno na ngozi yangu ilifanya mabakamabaka, pia nilikuwa na kikohozi kisichosikia dawa, ukichangia na lile donda la mgongoni ambalo lilikaribia kutapakaa mwili mzima, hata mimi nilijiona ni kama mfu aliye hai.

Ndugu zangu wakabishana sana baada ya maelezo yangu, wengine wakiona lilikuwa wazo zuri kwenda kutafuta tiba huku wengine wakiona kwenda huko ni kujiua kabla ya siku zangu za kufa kufika. “bora aendelee kuwa hapa hata kama akifa tutamzika kiheshima kuliko kujipeleka kufia mbali ambapo hatutoona hata mwili wake” alishauri baba yangu mdogo ambaye alikuwpo kwenye kikao kile.

“mimi nafikiri ni bora kufa ukipmbana kuliko kukaa kukingojea kifo” alishauri mdogo wangu na mke wangu akamuunga mkono, “anachokisema shemeji ni sawa ila anahitaji mtu wa kwendanae maana hali yake ya afya sio nzuri, mimi nitakwendanae” alisema mke wangu na kuzua mzozo, wengine wakisema aende huku wengine wakikataa “lazima aende, kwani mwenzie si alipata matatizo haya kwaajili ya kwenda kmsaidia yeye? Kwanini na yeye asimsaidie sasa?” alisema dada yangu ambaye hakuwahi kuwa na mapenzi ya dhati kwa wifi yake huyu. Mabishano ya hapa na pale yakaendelea lakini mimi nikajihisi mwili wangu ukiishiwa nguvu, hata mabishano yale nikawa nayasikia kwa mbali kama vile nilikuwa ndotoni, mara nikaanguka chini kama mzoga na sikujua nini kiliendelea tena.

Usikose sehemu ya 54


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here