SHARE

Waziri Wa mambo ya ndani ya nchi DK mwigulu Nchemba amewahakikishia usalama  wananchi wote ambao majimbo yao yanafanya uchaguzi  marudio na kuwataka kujitokeza Kwa wingi kupiga kura pasipo kuhofia usalama. wao.

Waziri Nchemba  amewaagiza vyombo vya ulinzi kuimalisha ulinzi siku ya uchaguzi na kwa yeyote atakaye leta fujo ili wananchi  wasiweze kwenda kupiga kura basi achukuliwe hatua za kisheria.

Akimnadi mgombea ubunge kupitia CCM  jimbo la Singida Kaskazini Justine Monko waziri Nchemba amesema anatosha kuwaletea maendelo zaidi kwani yule waliyemtuma mwanzo alichoka baada ya kufanya kazi kwa miaka mingi hivyo huyu anauwezo mkubwa wa kufanya kazi.

“CCM ina watoto wengi mmoja akisema amechoka baada ya kutumwa sana unamchukua mwingine na kumtuma, Monko anauwezo mkubwa wa kuwasaidia kuwaletea barabara na umeme ambao mmeukosa mpeni yeye atawasaidia” Waziri Mwigulu

Naye mgombea ubunge wa jimbo hilo Justine Monko amewataka wananchi kumpigia kura nyingi kesho ili aweze kuwaletea maendeleo kwa kuwajengea zahanati,barabara, na umeme ambao wameukosa kwa mda mrefu kwani anauzoefu ameshawai kuwa mkurugenzi wa halmashauri.

Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Singida Juma Kilimba amesema wanauwakika wa kushinda kwa asilimia kubwa hapo kesho kwani wamefanya kampeni kwa kata zote 21 na wananchi wanaimani kubwa na mgombea na Chama cha mapinduzi.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here