SHARE

Mchekeshaji Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Saalam baada ya kuugua.

Ofisa Habari wa Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni, Masoud Kaftany amethibitisha taarifa kuhusu kuugua kwa msanii huyo mkongwe.

Akiongea jana Alhamisi asubuhi, Kaftany amesema mwigizaji huyo alipelekwa hospitali hapo siku ya jana baada ya kuzidiwa.

“Ni kweli Mzee Majuto anaumwa na sasa hivi tupo naye hapa Muhimbili anaendelea na matibabu,” alisema Kaftany.

Aliongeza kuwa, “Kusema anaumwa nini ni mapema zaidi lakini baadaye tutatoa taarifa rasmi baada ya kupokea taarifa ya madaktari.”

Afisa huyo amekiomba Chama cha Waigizaji, wadau wa filamu Tanzania na Watanzania wote kumuombea muigizaji huyo aweze kupona haraka.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here