SHARE

Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea na msimamo wake wa kutishia kusitisha misaada kwa Taifa la Palestina endapo litakataa kushiriki kwenye mazungumzo ya amani.

Wizara ya Masuala ya Kigeni Marekani imethibitisha kwamba Trump alitoa msimamo huo alipokuwa akizungumzia kuhusu msaada wa kiuchumi na usaidizi wa kiusalama, ambapo aliituhumu Palestina kulivunjia heshima Taifa lake.

Msimamo huo umekuja ikiwa zimepita siku kadhaa tangu nchi ya Marekani kuzuia fedha kiasi cha dola milioni 65 zilizopangwa kwa ajili ya kulisaidia Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Palestina.

Hivi karibuni Palestina imeikataa Marekani kuwa mpatanishi asiyependelea upande wowote katika mazungumzo ya amani, kufuatia hatua ya Marekani kuutambua mji wa Yerusalem kama mji mkuu wa Israel.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here