SHARE

Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Bw. Daniel Zenda akikabidhi kadi 1500 za wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa Katibu wa Hamasa Seneti ya mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Juakali Kuwanya katika hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya UVCCM, Upanga  jijini Dar es Salaam.

Bw. Zenda amesema, kadi hizo amezikabidhi ili zigawiwe kwa wananchama wapya ambao wamekuwa wakijiunga kwa wingi katika Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake, kutokana na mwamko mkubwa wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuunga mkono CCM kutokana na kuvutiwa na Utendaji kazi wa awamu ya tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here