SHARE

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani utakaofanyika Februari 17, 2018 unakuwa wa amani na utulivu.

Akizungumza wakati akimnadi mgombea udiwani wa CCM Kata ya Madanga, Athumani Tunutu, Mwigulu amesema watakaofanya vurugu siku ya kupiga kura, watashughulikiwa.

Uchaguzi huo utafanyika katika majimbo ya Siha, Kinondoni na katika Kata 10.

“Tunawasikia baadhi ya viongozi wa vyama vya wenzetu wakiwahamasisha wananchi kukaa kwenye vituo vya kupiga kura baada ya kupigakura. Nikiwa kama waziri niliyepewa dhamana ya kuhakikisha ulinzi nawaonya msije kufanya hivyo, fuateni sheria inavyoeleza, ”amesema.

Amesema Serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru, kwamba ana amini mgombea wa CCM atashinda kutokana na wapigakura kujenga imani kubwa na Rais John Magufuli.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here