SHARE

Chadema imesema imeupokea ushauri uliotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa kuwa vyama vya upinzani vitafute ufumbuzi wa zuio la mikutano ya hadhara mahakamani badala ya kulalamika.

Dk Slaa ambaye ni balozi mteule alitoa ushauri huo  alipofanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Clouds.

Alipoulizwa kuhusu msimamo wa chama chake juu ya ushauri wa Dk Slaa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema  kuwa chama hicho kimeupokea ushauri huo na kitaufanyia kazi.

“Tumepokea ushauri wake, tunashukuru. Tutaufanyia kazi,” amesema Dk Mashinji alipojibu swali wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Katika mahojiano kwenye kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo hicho cha televisheni, Dk Slaa ambaye kwa sasa anaishi Canada alisema anaungana na wale wanaodai kuwapo kwa mikutano.

“Sikubaliana na taratibu zinavyosemwa, tumepigwa marufuku na mimi naungana nao kwa sababu mimi sikubaliani na jambo lililopitishwa na Bunge linaweza kuondolewa kwa kauli,” alisema.

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here