SHARE

Kocha Mkuu wa Gendamarie, Mvuyekure Issa amesema walifanya kila linalowezekana kupunguza idadi ya mabao ambayo wangefungwa na Simba.

Simba imeitwanga Gendamarie mabao 4-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mvuyekure amesema alikuwa na hofu, Simba ingeweza kuwafunga hata mabao 9-0

.

“Tunajua ubora wa Simba hata kama haijashiriki michuano ya kimataifa. Lakini tulipanga kuhakikisha hatufungwi mabao mengi na ikiwezekana, nasi tufunge.

“Kwa maana ya mipango tulikwenda tunavyotaka, lakini tuna kazi ngumu mechi ijayo,” alisema.

Mara kadhaa, wachezaji wa Gendamarie walikuwa wakijiangusha au kulala chini kupoteza muda.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here