SHARE

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amewataka madiwani wa vyama vya upinzani kujiunga na CCM ili waweze kushirikiana naye kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa ndiyo serikali iliyopo madarakani.

Mnyeti ameyasema hayo jana akizungumza katika mkutano wa hadhara kata ya Haydom wilayani Mbulu, ambapo amesema ni vyema madiwani wa CHADEMA wakajiunga na CCM kwani yupo tayari kupokea simu ya diwani wa CCM hata akipigiwa usiku wa manane, ili kumpa msaada lakini si diwani kutoka vyama vya upinzani.

Amesema diwani wa CHADEMA ni ngumu kufanikisha maendeleo ya wananchi kwa madai kuwa, hakuna ambaye atamsikiliza akiwasilisha hoja zake katika vikao vya halmashauri husika.

“Hata hapa Haydom najua ni ngome ya Chadema hata mwenyekiti wa kijiji namuona ana damu ya CCM, sasa ondokeni huko mje huku tutekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 kwa kuleta maendeleo,” amesema Mnyeti.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here