SHARE

Cyril Ramaphosa amechaguliwa na Bunge la Afrika Kusini kuwa Rais wa nchi hiyo baada ya Jacob Zuma kujiuzulu jana.

Zuma alikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa chama chake cha ANC kilichomtaka ajiuzulu la sivyo akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani dhidi yake bungeni.

Kupitia kituo cha Televisheni Zuma alisema kuwa anajiuzulu mara moja lakini hakubaliani na uamuzi wa chama.

Zuma nakabiliwa na madai kadhaa ya ufisadi lakini amekana kufanya makosa yoyote.

Zuma , mwanachama wa jeshi la ANC wakati wa ubaguzi wa rangi, alipitia nyadhfa kadhaa za chama hicho hadi kuwa rais.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here