SHARE

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ anatarajia kufanya ziara ya muziki kwenye majiji 12 nchini Marekani.

Ziara hiyo inatarajiwa kuanza Juni 22 hadi Julai 23, 2018 na itakuwa maalumu kwa ajili ya kuitangaza albamu yake ya A boy from Tandale ambayo itazinduliwa Machi 14.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa Diamond, Sallam Sharaff alisema, burudani itaanza katika jiji la New York, Los Angeles, Minnesota, Houston, Seattle, Kansas City, Washington DC, Boston, Atlanta, Columbus, Philadephia na Dallas.

“Hii itakuwa safari kwa ajili ya wimbo wake wa ‘A boy from Tandale’ baada ya kuachiwa rasmi Machi 14 nchini,” alisema.

Diamond anakuwa msanii wa pili kutangaza ziara ya kimataifa mwaka huu baada ya Aslay Isihaka kutangaza kufanya ziara katika bara la Ulaya kwenye nchi za Norway, Sweden, Finland, Uswisi, Ujerumani, Denmark na Holand kuanzia Machi 2 hadi Aprili 7 mwaka huu.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here