SHARE

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ anatarajia kuzunguka mikoani kwa ajili ya kutafuta watangazaji wa radio na runinga yake ya Wasafi.

Mwishoni mwa mwaka jana Diamond alitangaza kufungua radio na kituo cha runinga ambapo alisema zitakuwa zinaitwa Wasafi Radio na TV kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira kwa vijana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika “Please tell me, from your perspective which city has the best Radio and Tv presenters…? (Naomba mniambie mji upi una watangazaji wazuri wa redio na runinga)”.

Baada ya posti hiyo watu mbalimbali walipendekeza mikoa tofauti tofauti, miongoni mwao ni DJ Nicotrack ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Dj Show cha radio One, ambaye alipendeza mikoa ya Mbeya na Arusha.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here