SHARE

Mauzo ya Hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kuanzia wiki iliyoishia Machi 2 hadi 9, 2018 yameshuka kutoka Shilingi bilioni 2.9 hadi kufikia milioni 518, vile vile idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa katika soko hilo imeshuka kutoka hisa milioni 2.4 hadi hisa laki 6.9.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Masoko Mwandamizi DSE, Marry Kinabo wakati akitoa taarifa ya kila wiki ya mauzo ya soko hilo kwa wanahabari.

Pia, Kinabo amesema ukubwa wa mtaji wa kwa Sh. Bilioni 417 kutoka Trilioni 23.1 hadi Trilioni 22.7 punguzo hilo limetokana na kushuka kwa bei za hisa za kampuni ya National Media Group (NMG) kwa asilimia 8, Benki ya Biashara ya Kenya (KCB) 7% na Acacia Mining (ACA) 5%, wakati ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani ukibakia kwenye kiwango kile kile cha Sh. Trilioni 10.2.

Katika hatua nyingine, amesema kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa DSE kwa pointi 43 kutok pointi 2,405 hadi 2,362 kutokana na kushuka kwa bei za hisa za NMG, ACA, wakati kiashiria cha kampuni za ndani kikibaki kama awali kwenye wastani wa pointi 3893.

Kwa upande wa kiashiria cha sekta ya viwanda vile vile kimebaki kwenye wastani wa pointi 5365, kiashiria cha huduma za kibenki ba kifedha kikibaki kwenye wastani wa pointi 2463.

Kuhusu mauzo ya hati fungani katika wiki iliyopita, amesema yalipanda kutoka Bilioni 4 kwa wiki iliyoishia Machi 2, 2018 hadi kufikia bilioni 65 kwa wiki iliyoishia Machi 9 mwaka huu, baada ya kuuzwa kwa hatifungani 12 za serikali zenye jumla ya gharama ya Bilioni 65.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here