SHARE

UONGOZI wa Klabu ya Simba umefunguka kuwa umejipanga kika­milifu kuhakikisha wa­nazikwepa hujuma zote ambazo watafanyiwa na wapinzani wao Al Masry mara watakapoingia nchini Misri kwa ajili ya kwenda kuvaana na klabu hiyo.

Simba wanatarajiwa kukwea pipa na kuwafuata Al Masry keshokutwa Jumatano kwa ajili ya kwenda kurudiana nao kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kucheza nao jijini Dar na kutoka nao sare ya mabao 2-2.

Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu, Kaimu wa Simba, Salim Ab­dallah ‘Try Again’ amese­ma kwamba wanajua safari yao ya Misri itakuwa na hujuma na figisu nyingi kutoka kwa wapinzani wao kwa ajili ya kuwatoa kwenye akili ya mchezo lakini wao wamejipanga kukabiliana na jambo hilo ili kutimiza lengo la ku­waondosha Waarabu hao kwenye michuano hiyo.

“Sisi kama viongozi tunajipanga vilivyo kuhak­ikisha kwamba mchezo ujao tunafanya vyema na kusonga mbele, tunajua kwamba wapinzani wetu wakiwa kwao wanakuwa na hujuma nyingi sana nje ya uwanja za hapa na pale kwa ajili ya kuwaondoa tu msiwe na mawazo ya mechi, lakini tunajipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba tunapambana nazo.

“Kwa mikakati ambayo tunaendelea kuiweka tunaamini kwamba tuta­fanya jambo kubwa kwa kuwasukuma nje wapin­zani wetu tukiwa huko­huko ugenini na jambo hilo linawezekana kwa sababu sisi kama uongozi tunatimiza majukumu yetu kwa asilimia zote kuiandaa timu kwa ajili ya mchezo huo muhimu,” alisema Try Again.

Simba wanaofundishwa na Mfaransa Pierre Lechantre watarudiana na Al Masry Machi 17, mwaka huu nchini Misri ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili wa kombe hilo la Shirikisho.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here