SHARE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo tarehe 14 Machi, 2018 ataweka jiwe la msingi katika sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” inayoanzia Morogoro hadi Makutupora Mkoani Dodoma.

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi zitafanyika leo kuanzia saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha Ihumwa nje kidogo ya Mji wa Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wananchi wa Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli hapa nchini Bw. Masanja Kadogosa anasema maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi katika sherehe hizo yamekamilika na amewataka wananchi kujitokeza katika sherehe na waliombali na Dodoma kufuatilia matangazo yatakayorushwa hewani na vituo vya redio na televisheni

Hii ni sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kati ya awamu tano zilizopangwa kukamilisha ujenzi wa reli hiyo itakayoanzia Dar es Salaam hadi Mwanza.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here