SHARE

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa amesikitishwa na matamshi ya msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakati akihojiwa na mtangazaji wa Times FM, Lil Ommy, kwa hatua ambazo Wizara inachukua kulinda maadili ya Kitanzania katika tasnia ya sanaa.

Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo na wasanii wawili kwa kukiuka maadili, yalifanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza anayemlaumu. Diamond atambue kuwa Serikali ina taratibu zake. Maamuzi ya Naibu Waziri ni maamuzi ya Wizara.

Kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, however popular he is. Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake.

Si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here