SHARE

Waasi waliojihami kwa silaha wamemuua mwanajeshi mmoja baada ya kushambulia nyumba ya Rais Joseph Kabila iliyoko eneo lenye mgogoro la Mashariki ambako mapigano hutokea mara kwa mara, wanajeshi walisema Alhamisi.

Kabila hakuwepo kwenye nyumba hiyo wakati wanamgambo wa Mai-Mai waliposhambulia nyumba hiyo karibu na mji wa Beni na wakakabiliana na wanajeshi wa serikali waliomudu kuzima shambulio.

Hili ni shambulio la pili kwa nyumba za rais katika muda wa miezi mitatu jambo ambalo ni kielelezo cha kuzidi kuzorota kwa hali ya usalama nchini DR Congo kwa upande mmoja kiini kikiwa hatua ya Kabila kukataa kujiuzulu mwaka 2016 kipindi chake cha uongozi kilipoisha.

Nyumba hiyo inayomilikiwa na Kabila ilishambuliwa na kuchomwa moto katika jimbo na Kivu Kaskazini Desemba mwaka jana. Polisi aliuawa katika shambulio hilo.

Hali ya usalama mashariki kwa nchi, eneo lililogeuka kuwa la mapigano ya kikabila, imezorota mwaka huu kutokana na mamlaka za serikali kuteleza hali iliyolazimu makumi kwa maelfu ya watu kukimbilia nchi jirani na kutishia kuivuruga nchi nzima.

Msemaji wa waasi wa Mai-Mai alisema wameua askari watatu katika shambulio hilo. Lakini msemaji wa jeshi la serikali amesema mmoja wa askari wao na mshambuliaji mmoja wameuawa.

Mai-Mai ni kundi la wanamgambo kwa asili lililoanzishwa kuzuia uvamizi wa Rwanda miaka ya 1990.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here